Aliyekuwa
Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema kupitia CHADEMA, amepoteza kiti hicho kwa
kuenguliwa na Mahakama katika kesi iliyokuwa inamkabili ya kupinga ubunge wake
alioupata mwaka 2010.
Kesi hiyo iliyofunguliwa na makada watatu wa CCM, Mussa Mkanga (55), Happy Kivuyo (49) na Agnes Mollel (44) ambao walikuwa wanamtuhumu Mbunge huyo kwa kutoa kauli za udhalilishaji, matusi na kashifa kwa aliyekuwa mgombea wa Ubunge jimbo hilo kwa tiketi ya CCM, Dkt. Batilda Buriani. Hukumu hiyo iliyosomwa na Jaji Mfawidhi wa Kanda ya Sumbawanga, Gabriel Rwakibarila.
Katika hukumu hiyo, Lema hakuondolewa haki ya kugombea ubunge huo kwa kuwa kosa lililomtia hatiani ni matumizi mabaya ya lugha tofauti na ilivyodhaniwa kuwa ni vitendo vya rushwa.
No comments:
Post a Comment