Msishangae

Wednesday, March 28, 2012

CBE: No vimini, milegezo

CHUO cha Elimu ya Biashara (CBE) kimepiga marufuku uvaaji wa milegezo na vimini, wanaume kusuka nywele na vitendo vingine vinavyokiuka utamaduni, mila na desturi za kiafrika chuoni kwa kusisitiza kuwa vinachangia wanafunzi wengine kutozingitia au kutokuwa makini kwenye masomo darasani. Mwanafunzi atakayekiuka sheria ya chuo inayokataza uvaaji wa mtindo huo atafukuzwa chuo pamoja na adhabu nyingine ambazo chuo kitaona zinafaa.
Kaimu Mkuu wa Chuo hicho, Athuman Ally Ahmed ametangaza uamuzi huo wa chuo na ametoa muda wa wiki chache kuhakikisha wanafunzi wanaachana na mitindo hiyo.
CBE wameonesha njia, wengine wafuate.

No comments:

Post a Comment