Msishangae

Sunday, February 22, 2015

Wiki iliyipita Rais Jakaya Kikwete alifanya uteuzi wa wakuu wa wawilaya. Katika idadi ya wakuu 133, kati yake 27 wameteuliwa wapya, 64 wamehamishwa vituo vya kazi na 42 wamebaki katika vituo vyao vya zamani. Katika uteuzi huo, waliokuwapo 12 wameteunguliwa uteuzi na wengine saba watapangiwa kazi nyingine. Katika uteuzi huo, Mwandishi wa Habari wa TBC Shaban Kissu amechaguliwa kuwa mkuu wa wilaya ya Kondoa na Kada wa UV-CCM Makonda ni DC Kinondoni. na Wilayani Makete anakwenda Muyingo Rweyimamu.

Monday, February 9, 2015

Safar ya Vicoba Jozan
Mfinde na Mpango wa kununua ndizi baada ya kurudi kutoka Jozan.


Wednesday, October 8, 2014

Watoto wa Idinepha walipocheza katika uzinduzi wa kikundi hicho Tazara.


migogoro ya ardhi

Serikali yapata suluhisho kuhusu migogoro ya ardhi kwa kuamua kupima ardhi na kuwapa hati za kumiliki za kimila wenye maeneo yaliyopimwa. Wilaya ya Mvomero ndiyo imechaguliwa kuwa ya majaribio na kampeni ikifanikiwa kuzima migogoro basi mtindo huo utatumika katika wilaya na maeneo mengine yenye migogoro.


Rasimu iliyopendekezwa


Marais Jakaya Kikwete na Mohamed Shein leo wanapokea RASIMU ya Katiba iliyopendekezwa na Mbuge Maalum la Katiba chini ya Mwenyekiti wake, Samuel Sitta na msaidizi wake Samia Suluhu. Kupokea rasimu hiyo kunakamilisha mchakato huo kinachobaki ni wananchi kupigia kura rasimu hiyo. Tukio hilo ni la kihistoria katika Tanzania.

Tuesday, September 9, 2014


Mashine za Kisasa za Ebola zafungwa katika Viwanja vya Ndege vya Dar es Salaam, Mwanza, Zanzibar na Kilimanjaro. Uwezo wa mashine hizo ni mkubwa kiasi cha kuweza kubaini dalili za ebola mwilini mwa binadamu.